Friday, 27 March 2009

DALILI ZA UJAUZITO

Watu wengi wamekuwa wakichanyikiwa na dalili za ujauzito leo nimeamua niwaletee dalili hizi
Dalili za kwanza za msichana au mwanamke kuwa na ujauzito ni zipi?
1.Dalili moja iliyo wazi zaidi ni kukosa hedhi muda unaotakiwa, mara nyingi ina maana kwamba amepata mimba.
2.Dalili nyingine ni kuvimba matiti na chuchu kuchomachoma. Baadhi ya wanawake wanaota nywele nyingi sehemu za siri na wengine wengi rangi ya chuchu inabadilika kuwa nyeusi.
3.Karibu nusu ya wanawake wajawazito huumwa tumbo na wengine hutapika.
4.Kusikia mkojo mara kwa mara.
5.Kujisikia uchovu.
6. kuona kizunguzungu, hasa katika miezi mitatu ya mwanzo hali hii inawapata baadhi ya wanawake na sio wote.
7.Kupenda au kuchukia baadhi ya vyakula.
8.Kusikia kichefuchefu.
9.Kuvimba fizi na meno kuuma wakati mwingine meno hutoa damu wakati wa kupiga mswaki.
Ili kuwa na uhakika kama ni mjamzito au hapana, unaweza kwenda kupima mkojo kwenye kliniki,hospitalini au ukanunua kipimo cha ujauzito na ukapima mwenyewe.

No comments:

Post a Comment